Home >  Term: marekebisho ya katiba
marekebisho ya katiba

Mageuzi ama nyongeza inayofanyiwa katiba. Ingawa marekebisho 6,000 kwa katiba ya Marekani yameweza kupendekezwa kwenye bunge la Congress, ni 27 tu ambayo yameweza kutekelezwa na la hivi karibuni likiwa mwaka 1992. Kwa mujibu wa katiba, kuna njia nne ambapo katiba inaweza kufanyiwa marekebisho. Marekebisho huweza kupendekezwa kwa majimbo baada ya thuluthi mbili ya kura kwenye bunge zote za Congress ama kwa thuluthi mbili ya kura kwenye bunge za majimbo. Mara tu inapopendekezwa kwa majimbo, inaweza kuridhiwa na bunge za robo tatu ya majimbo ama kwa mikutano kwenye robo tatu ya majimbo. Marekebisho yote 27, isipokuwa la 21,yaliweza kupendekezwa na thuluthi mbili ya wajumbe kwenye bunge la Congress na kuridhiwa na robo tatu ya bunge za majimbo.

0 0

Creator

  • Jonah Ondieki
  • (Nairobi, Kenya)

  •  (Bronze) 283 points
  • 100% positive feedback
© 2025 CSOFT International, Ltd.